Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Wanajeshi wa MarekaniPicha: Daniel Karmann/dpa/picture alliance
Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kwamba kupelekwa kwa wanajeshi hao kutaongeza idadi ya timu ndogo ambayo tayari iko nchini Nigeria ili kusaidia katika kutoa mafunzo,mwongozo wa kiufundi na kufanya mashambulizi.
Kamandi ya jeshi la Marekani ya Afrika imesema kwamba Marekani itapeleka wanajeshi 200 nchini Nigeria kutoa mafunzo kwa jeshi la nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika katika mapambano yake dhidi ya makundi ya kigaidi.
Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kwamba kupelekwa kwa wanajeshi hao kutaongeza idadi ya timu ndogo ambayo tayari iko nchini Nigeria ili kusaidia katika kutoa mafunzo,mwongozo wa kiufundi na kufanya mashambulizi.
Utawala wa Trump umekuwa ukisisitiza kuwepo kwa matukio ya kulengwa na kuuliwa kwa Wakristo nchini Nigeria ingawa Nigeria yenyewe imekuwa ikakanusha madai hayo na kusema kwamba jamii zote mbili za waikristo na waislamu ni wahanga wa matukio hayo ya kigaidi.
Kwa miaka mingi Nigeria imekuwa ikipambana na makundi ya kijihadi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ambayo yamekuwa yakiua, yakiteka nyara, kupora na kudai fidia.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.