Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Picha ya setlaiti inaonesha kimbunga MadagascarPicha: DEFIS_EU/REUTERS
Takriban watu 20 wamefariki dunia huko Madagascar kufuatia kimbunga kilichosababisha upepo mkali ulioharibu mapaa ya nyumba na kusababisha mafuriko.
Haya yamesemwa na mamlaka ya kusimamiamajanga katika kisiwa hicho kilichoko Bahari Hindi.
Mamlaka hiyo imesema watu 15 hawajulikani walipo na angalau wengine 33 wamejeruhiwa. Kimbunga Gezani kilitua Madagascar jana Jumanne katika mji wa pili mkubwa Toamasina, huku upepo ukipiga kwa kasi ya kilomita 250 kwa saa.
Wakaazi wa mji huo wameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa, upepo huo mkali umesababisha kuta za mawe kuanguka. Kiongozi mpya wa nchi hiyo Kanali Michael Randrianirina aliyechukua mamlaka mwezi Oktoba, alikuwa mjini humo kutazama hali na uharibifu uliofanyika.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.