Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Ubalozi wa Canada huko GreenlandPicha: Florent Vergnes/AFP
Jumuiya ya Kujihami ya NATO inaongeza uwepo wake katika eneo la Arctic na maeneo ya karibu.
Hii ni kufuatia mzozo kuhusiana na kisiwa cha Greenlandkusababisha mpasuko kati ya Marekani na washirika wake wa Ulaya.
Kulingana na Kamanda wa Ulaya Alexus Grynkewich, mpango huo ujulikanao kama Arctic Sentry utatumia nguvu ya NATO kuhakikisha eneo hilo linasalia kuwa salama.
Kuongeza uwepo wa NATO huko Greenland ni jambo lililopendekezwa na baadhi ya mataifa ya Ulaya ili kupunguza mzozo kukihusu kisiwa hicho, ambacho Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kukitwaa akisema asipofanya hivyo, basi Urusi au China ndio watakaokiteka.
Baada ya mkutano na Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte katika Jukwaa la Kiuchumi Duniani lililofanyika huko Davos, Uswisi mwezi uliopita wa Januari, Trump alitangaza kuwa tayari kuna rasimu ya makubaliano ya baadae kuhusu Greenland na eneo zima la Arctic.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.