Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Rais wa Misri Abdel Fattah al-SissiPicha: John Macdougall/AP Photo/picture alliance
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amewaapisha mawaziri wapya Jumatano kufuatia mabadiliko ya baraza lake la mawaziri yaliyoshuhudia mabadiliko ya dakika ya mwisho katika wizari ya ulinzi.
Mabadiliko hayo yamezilenga wizara za uchumi na ulinzi wakati nchi hiyo inapojaribu kujiondoa kutoka kwenye mgogoro wa kiuchumi wa miaka kadhaa.
Sisi amemteua waziri mpya wa ulinzi Jenerali Ashraf Salem Zaher asubuhi ya Jumatano wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa mawaziri hao.
Anaichukua nafasi ya Abdelmaguid Saqr na ataiongoza wizara ya ulinzi na uzalishaji wa kijeshi.
Awali wizara ya uzalishaji wa kijeshi nchini Misri ilikuwa ya kujitegemea na ilisimamia uchumi wa jeshi. Kulingana na taarifa kutoka ofisi yake, Rais Sisi ameiagiza wizara ya uchumi kushughulikia kulipunguza deni la taifa.
Misri ambayo ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya watu katika ulimwengu wa kiarabu, imepitia kipindi kigumu ikiwemo sarafu yake kushuka thamani mara tano katika kipindi cha mwongo mmoja.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.