Ofisi ya haki za binadamu ya UN kufunguliwa tena Venezuela

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Shirika la haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa linanuia kufungua upya ofisi zake mjini Caracas, VenezuelaPicha: Fatih Erel/AA/picture alliance

Shirika la Haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa limesema hii leo kwamba liko kwenye mazungumzo na Venezuela ya kufungua upya ofisi yake nchini humo, miaka miwili baada ya kufukuzwa.

Msemaji wa shirika hilo Ravina Shamdasani amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba, mkuu wa shirika hilo Volker Turk aligusia hilo alipozungumza na rais wa mpito wa Venezuela Delcy Rodriguez Januari 26.

Amesema kwenye mazungumzo yao Turk alimuahidi rais huyo wa mpito kuisaidia Venezuela kuandaa mpango wa mazungumzo na maridhiano, ambapo suala la haki za binadamu litatiliwa kipaumbele.

Akaongeza pia ana nia ya kufungua upya ofisi za shirika hilo na tayari alituma timu iliyozuru Caracas hadi Februari 4, ambayo ilikutana na makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na watetezi wa haki za binaadamu.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment