Ikulu ya Kremlin yasema iko tayari kuzungumza na Macron

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema anaamini Ulaya inapaswa kwa mara nyingine kuzungumza moja kwa moja na Rais wa Urusi Vladimir Putin kama moja ya juhudi za kusaka suluhu ya amani katika vita vya nchini Ukraine.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameitaka Ulaya kufanya mazungumzo mapya na rais wa Urusi, Vladimir Putin ya kuvimaliza vita nchini UkrainePicha: Romain Doucelin/SIPA/picture alliance

Macron amesema katika mahojiano na magazeti kadhaa ya Ulaya yaliyochapishwa hii leo kwamba Ulaya haipaswi kuwaachia Urusi na Washington mazungumzo hayo.

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amethibitisha kuwepo kwa mawasiliano na kusema Urusi iko tayari kurejea kwenye mazungumzo na Ufaransa, katika ngazi ya rais.

“Tunaweza kuthibitisha kwamba kumekuwepo na mawasiliano, ambayo ikiwa yatahitajika na ni lazima yanaweza kusaidia kuanzisha mara moja mazungumzo ya ngazi za juu. Hadi sasa, hatujaona nia yoyote, ingawa tumeona kauli ya Macron kuhusu hitaji la kuanzisha uhusiano na Urusi.”

Rais Vladimir Putin mara kadhaa ameitetea Urusi kwamba haikuvunja uhusiano, bali ni mataifa ya Ulaya.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment