Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA

Vikosi vya usalama vya Israel vikishika doria Ukingo wa MagharibiPicha: HAZEM BADER/AFP
Mamlaka ya Palestina imeripoti kuwa wanajeshi wa Israel wamewaua wavulana wawili wa Kipalestina wenye umri wa miaka 15 katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Kwa upande wake, Israel imewataja wavulana hao kuwa ni “magaidi” waliokuwa wakielekea kufanya shambulio.
Katika taarifa yake, jeshi hilo la IDF lilisema “askari wake waliokuwa wakifanya operesheni karibu na jamii ya Karmei Zur waliwaua magaidi wawili waliokuwa njiani kwenda kufanya shambulio la kigaidi.”
Hata hivyo, jeshi hilo halikutoa maelezo zaidi huku mamlaka ya Palestina pia haikutoa taarifa ya ziada kuhusu tukio hilo.
Mauaji ya wavulana hao wawili yametokea wakati ambapo mivutano kati ya walowezi wa Israel na raia wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi imeongezeka kwa kasi katika wiki za hivi karibuni, hali ambayo imezua shutuma kali na hata ukosoaji wa nadra kutoka ndani ya jeshi na serikali ya Israel.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.