Ripoti yafichua usafirishaji wa mafuta kwa RSF kutoka Libya

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Raia wa Sudan akisherehekea na wanajeshi kufuatia tangazo la jeshi kwamba lilitwaa mji wa Wad MadaniPicha: Ibrahim Mohammed Ishak/REUTERS

Vikosi vinavyomuunga mkono mbabe wa kivita nchini Libya Khalifa Haftar vinaripotiwa kusafirisha mafuta kwa njia ya magendo na kuwapelekea wanamgambo wa RSF nchini Sudan kwa niaba ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa jana na shirika la uangalizi la The Sentry, lenye makao makuu yake nchini Marekani. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Khalifa Haftar “amekuwa msambazaji muhimu wa mafuta kwa wanamgambo wa RSF” katika kipindi chote cha vita, hali inayodaiwa kuchangiwa na “uaminifu wake kwa serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu.”

Umoja wa Mataifa umeituhumu Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kuipatia RSF silaha, droni na vifaa vingine vya kijeshi, tuhuma ambazo UAE imekanusha mara kadhaa.

Vita kati ya jeshi la serikali ya Sudan na wanamgambo wa RSF vilianza mnamo Aprili 2023, na vimesababisha vifo vya maelfu ya watu.

Takriban watu milioni 12 wamelazimika kuyakimbia makaazi yao nchini Sudan na mzozo huo umetajwa kuwa miongoni mwa migogoro mikubwa zaidi ya kibinadamu duniani.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment