Rais wa Tanzania Samia Suluhu kulihutubia bunge la 13

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Rais wa Tanzania Samia Suluhu HassanPicha: Michael Jamson/AFP

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa leo kulihutubia bunge, ikiwa ni ishara ya kulizindua rasmi baada ya kukamilika kwa uteuzi wa viongozi wake wakuu, wakiwemo Waziri Mkuu, Spika wa Bunge na Naibu Spika.

Hotuba ya Rais Samia Suluhu inatarajiwa kueleza vipaumbele vya serikali yake kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, ikiwemo mikakati na ajenda za maendeleo, mwelekeo wa demokrasia na juhudi za kuimarisha umoja wa kitaifa.

Wananchi, wanadiplomasia na wachambuzi wa kisiasa wanasubiri kwa shauku kubwa hotuba hiyo, hasa ikizingatiwa ukosoaji wa kimataifa hivi karibuni kuhusu mchakato wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 pamoja na maandamano yaliyoshuhudiwa nchini humo.

Bunge la 13 la Tanzania limeundwa baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 ambao ulizua mjadala mkubwa kuhusu uwazi na ushirikishwaji wa vyama vya upinzani.

Rais Samia alishinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 97.66 ya kura.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment