China yamuita balozi wa Japan kufuatia kauli ya Takaichi

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Rais wa China Xi Jinping akisalimiana na Waziri Mkuu wa Japan Sanae TakaichiPicha: Kaname Yoneyama/AP Photo/picture alliance

Serikali ya China imesema leo kuwa imemuita balozi wa Japan katika ofisi yao ya wizara ya mambo ya nje ili kutoa ufafanuzi kufuatia matamshi ya Waziri Mkuu mpya wa Japan Sanae Takaichi kuhusu Taiwan.

Wiki iliyopita, Takaichi aliwaambia wabunge wa Japan kwamba mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Taiwan yanaweza kuhalalisha hatua ya kutuma wanajeshi wa Japan kusaidia kisiwa hicho, chini ya kanuni ya “utetezi wa pamoja.”

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imekosoa vikali kauli hiyo, ikisema kuwa “haitovumilia kabisa” matamshi kama hayo.

Msemaji wa wizara hiyo, Lian Jian, amewaambia waandishi wa habari kuwa Japan “lazima irekebishe makosa yake mara moja na iondoe matamshi yasiyo na msingi.”

China inasisitiza kuwa Taiwan ni sehemu ya himaya yake na serikali ya Beijing haijaondoa uwezekano wa kutumia nguvu kuirejesha Taiwan chini ya udhibiti wake, licha ya kisiwa hicho kuwa na utawala wa ndani unaojitegemea.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment