Serikali yasema zaidi ya Wakenya 200 wamesajiliwa katika jeshi la Urusi

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na :Cantona Joseph|RFA

.
Maelezo ya picha,Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi

Zaidi ya Wakenya mia mbili huenda wamejiunga na jeshi la Urusi tangu kuanza kwa mzozo kati ya Urusi na Ukraine mnamo 2022, Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi amesema.

Akizungumza na wanahabari, Mudavadi alisema wizara hiyo imeendelea kupokea maswali kutoka kwa familia zinazotaka kujua waliko jamaa zao ambao walijikuta katika mzozo huo.

“Ripoti zinaonyesha kuwa zaidi ya Wakenya mia mbili huenda wamejiunga na jeshi la Urusi, huku wengine wakiwa wanachama wa zamani wa huduma za nidhamu za Kenya,” alisema Waziri huyo, akiongeza kuwa zoezi la usajili nchini Urusi limeripotiwa kupanuka na kujumuisha raia wa Kiafrika, ikiwa ni pamoja na Wakenya.

Mudavadi alibainisha kuwa inakadiriwa kwamba mitandao ya usajili ingali inaendelea na kazi hiyo nchini Kenya na Urusi, huku Ubalozi wa Kenya mjini Moscow ukiripoti wale waliopata majeraha na huku wengine wakiwa wamekwama baada ya kujaribu kujisajili kuingia vitani.

Jamii ya kimataifa ichukue hatua kukomesha usambazaji silaha kwa RSF, asema Rubio

.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, ametoa wito wa hatua za kimataifa kuchukuliwa kukomesha usambazaji wa silaha kwa vikosi vya Rapid Support Forces (RSF, akilaumu kundi hilo kwa umwagaji damu na kusema kuwa kinachoendelea nchini Sudan kwa sasa ni ‘janga’.

“…Hatua inastahili kuchukuliwa kukomesha usambazaji wa silaha na msaada ambao RSF inapata wakati inaendelea vitendo vyake vya ukatili…,” alisema Rubio.

Rubio pia aliangazia viwango vya utapia mlo ambavyo vimerekodiwa akisema kuwa havijawahi kushuhudiwa hapo kabla kulingana na mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu yaliopokea baadhi yao kama wakimbizi huku kukiwa na hofu ya wale ambao wamesalia nchini humo.

“Idadi ndogo ya wanaojitokeza kama wakimbizi inazua maswali mengi. Watu wamefariki dunia au wameshindwa kutembea,” Rubio aliongeza wakati akizungumza na wanahabari.

Rubio alirejelea wito wa kusitishwa kwa mapigano na pande zote mbili ambao unaonekana kutoheshimiwa na kuendeleza vitendo vya kikatili vinavyoonekana kufanywa kwa mpangilio uliopangwa ili kuficha ukweli.

“Sio kwamba wanapigana vita tu jambo ambalo tayari ni baya, wanatekeleza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, mauaji, vitendo vya kutisha dhidi ya kina mama, watoto na raia wasio na hatia, hili linastahili kukomeshwa mara moja,” amesema Waziri Rubio.

Alihakikisha kuwa kuna majadiliano na nchi na washirika mbali mbali kusitisha vitendo vya kikatili nchini Sudan vinavyotekelezwa na RSF.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment