Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na :Cantona Joseph|RFA

German Galushchenko, mshirika mkuu wa Rais wa Ukraine anadaiwa kuanzisha mpango wa ufisadi wa dola milioni 100 katika sekta ya nishati Ukraine.Picha: Danylo Antoniuk/Ukrinform/IMAGO
Mawaziri wa sheria na nishati nchini Ukraine, German Galushchenko na Svitlana Hrynchuk, wamejiuzulu jana Jumatano kufuatia madai ya kuhusika kwao na sakata kubwa la ufisadi katika sekta ya nishati nchini humo.
Wachunguzi wamedai kuwa Galushchenko, mshirika mkuu wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, alianzisha mpango wa ufisadi wa dola milioni 100 katika sekta hiyo, hali iliyosababisha hasira ya wananchi wakati ambao taifa linakosa umeme kufuatia mashambulizi ya Urusi yanayoendelea kushamiri huko.
Ukraine imekuwa ikikabiliwa na kashfa mbalimbali za ufisadi, na kuondoa tatizo hilo serikalini ni moja ya masharti yanayohitajika ili kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Awali Rais Zelensky aliwataka mawaziri hao kujiuzulu kufuatia uchunguzi wa sakata ya hilo ufisadi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.