Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na :Cantona Joseph|RFA

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, Marco Rubio amesema nchi yake ina matumaini kuhusu azimio la UN kuhusu amani ya GazaPicha: Fadel Senna/UPI Photo/IMAGO
Marekani kupitia waziri wake wa mambo ya nchi za nje Marco Rubio, imesema ina matumaini kwamba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakamilisha azimio kuhusu Gaza.
Azimio hilo linaunga mkono hatua ya kupelekwa kwa kikosi cha kimataifa cha kulinda amani.
Rubio amesisitiza kuwa hatua muhimu zinapigwa na muafaka utapatikana hivi karibuni.
Huku hayo yakijiri, Rais wa Israel Isaac Herzog, pamoja na maafisa waandamizi wa jeshi, wamelaani vitendo vya walowezi wa Kiyahudi dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu, wakitaka kukomeshwa mara moja vitendo hivyo vinavyoongezeka.
Herzog aliyaelezea mashambulizi hayo kama “ya kushangaza na “makubwa”. Naye Marco Rubio amesema vurugu hizo zinaweza kuathiri mpango wa amani wa Gaza.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.