Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na:Cantona Joseph|RFA

Magari ya shirika la msalaba mwekundu yanayotumiwa kubebea miili ya mateka inayorejeshwa IsraelPicha: Dawoud Abu Alkas/REUTERS
Tawi la kijeshi la Hamas limesema litaurejesha mwili wa mateka mwengine hii leo kama sehemu ya mpango wa usitishwaji mapigano Gaza uliosimamiwa na Marekani.
Tawi hilo la Al-Quds Brigades na jengine la Ezzedine al-Qassam Brigades yataurejesha mwili huo uliopatikana katika eneo la Morag, kaskazini mwa mji wa Khan Yunis Kusini mwa Ukanda wa Gaza.
Taarifa ya Hamas imesema kati ya miili 28 iliyopaswa kuirejesha Israel chini ya mpango huo ulioanza kutekelezwa Oktoba 10, tayari imesharejesha miili 24.
Israel nayo, kwa upande wake imewaachia wafungwa takriban 2,000 wa Kipalestina waliokuwa wanazuiliwa nchini humo na kurejesha miili ya mamia wengine.
Israel imedai kuwa Hamas inajikokota kuirejesha miili ya mateka, lakini Hamas nao wanasema hilo linatokea kwa sababu miili mingi imefukiwa chini ya vifusi vya majengo yaliyoshambuliwa na Israel yaliyolikumba eneo hilo kwa miaka miwili.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.