Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na :Cantona Joseph|RFA

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zilizoendelea kiviwanda duniani G7 katika picha ya pamojaPicha: Mandel Ngan/AFP
Katika mkutano uliofanyika nchini Canada, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zilizoendelea kiviwanda duniani G7 wametoa wito wa dharura wa kusitishwa kwa vita vinavyoendelea nchini Ukraine.
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zilizoendelea kiviwanda duniani G7 wametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa vita vinavyoendelea nchini Ukraine.
Katika tamko la pamoja, mawaziri kutoka Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, na Marekani wameeleza kuunga mkono kwa dhati uhuru wa Ukraine, huku wakionyesha wasiwasi kuhusu kuzorota kwa hali ya usalama nchini Sudan.
Mazungumzo hayo yalifanyika karibu na maporomoko maarufu ya maji ya Niagara Falls, ambapo viongozi hao walijadili mikakati ya kuimarisha ufadhili kwa juhudi za Ukraine kupambana dhidi ya uvamizi wa Urusi.
Miongoni mwa ajenda kuu zilizojadiliwa ni pendekezo la “kutumia zaidi mali za serikali ya Urusi zilizozuiliwa” katika nchi mbalimbali za G7 — mkakati tata unaoendelea kujadiliwa kwa kina ndani ya Umoja wa Ulaya.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.