Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na :Cantona Joseph|RFA

Kiongozi wa serikali ya mpito Bangladesh Muhammad Yunus, amesema nchi yake inaandaa kura ya maoni kuhusu mageuzi ya kitaifaPicha: Bangladesh CA Press wing
Kiongozi wa serikali ya mpito Bangladesh Muhammad Yunus, amesema nchi hiyo inaandaa kura ya maoni kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya mwezi Julai ya kuwa na mageuzi ya kitaifa, yaliyoandaliwa baada ya maandamano makubwa
Kiongozi wa serikali ya mpito Bangladesh Muhammad Yunus, amesema nchi hiyo iliyoko bara Asia inaandaa kura ya maoni kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya mwezi Julai ya kuwa na mageuzi ya kitaifa, yaliyoandaliwa baada ya maandamano makubwa ya wanafunzi, yaliyofanyika mwaka uliopita.
Kiongozi huyo pia amesema kwamba uchaguzi wa bunge utafanyika mwezi Februari na utakuwa wa huru na haki.
Makubaliano ya Julai yanalenga, kubadilisha siasa na taasisi za taifa hilo na utambuzi wa katiba kwa maandamano ya 2024 yaliyomlazimisha Sheikh Hasina waziri mkuu wa muda mrefu nchini humo kuitoroka nchi na kukimbilia uhamishoni nchini India.
Vyama vingi vya kisiasa vilitia saini makubaliano hayo mwezi Oktoba, lakini chama cha National Citizens, kilichoundwa na viongozi wa vuguvugu la mwaka uliopita pamoja na vyama vingine vinnne vya mrengo wa kushoto vilisusia makubaliano hayo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.