Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Wanajeshi wa UturukiPicha: Umit Kozan/Depo Photos/ZUMA/dpa/picture alliance
Wanajeshi 20 waliokuwa kwenye ndege ya kijeshi ya Uturuki wamefariki dunia baada ya ndege hiyo kuanguka katika eneo la mpaka wa georgia na Azerbaijan hapo Jumanne.
Wizara ya ulinzi ya Uturuki mapema Jumatano imechapisha picha za wanajeshi hao 20 waliofariki dunia katika mtandao wa kijamii wa X.
Shirika la habari la Uturuki Anadolu limeripoti kuwa sababu ya ajali hiyo ya ndege bado haijajulikana.
Ndege hiyo ilikuwa inatoka Azerbaijan kuelekea Uturuki na kulingana na wiazara ya mambo ya ndani ya Uturuki, ilianguka karibu kilomita tano tu kutoka mpaka wa Azerbaijan.
Mamlaka zinachunguza iwapo ukiukaji wa sheria za usafiri wa angani ulichangia ajali hiyo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.