Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Noël Barrot, ameonya kuhusu hatua za Marekani kwenye eneo la Karibi.Picha: Stephane Lemouton/SIPA/picture alliance
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amezikosowa operesheni za kijeshi kwenye eneo la Karibi, ambako Marekani imetuma meli zake za kijeshi ka madai ya kukabiliana na magenge ya madawa ya kulevya ya Venezuela.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye siku ya awali ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa kundi la G7 wanaokutana nchini Kanada, Jean-Noel Barrot amesema ni muhimu sana kuepuka hatua zozote zinazochochea machafuko na makabiliano, baada ya Venezuela kuonya kwamba hatua za Marekani zinaweza kupelekea vita.
Bila kuitaja Marekani, Barrot amesema nchi yake inafuatilia operesheni hizo za kijeshi ambazo zinakiuka sheria ya kimataifa.
Kauli hiyo imekuja baada ya meli kubwa kabisa ya kijeshi ya Marekani, USS Gerald R. Ford, kuingia kwenye eneo linalodhibitiwa na Kamandi ya Kusini ya Jeshi la Majini la Marekani linalojumuisha Amerika Kusini na Karibi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.