TLS yazungumzia kesi za uhaini Tanzania

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Mfanyabiashara wa Tanzania Jeniffer Jovin “Niffer” ni miongoni mwa washitakiwa wa uhaini nchini humoPicha: Ericky Boniphase/DW

Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kimetoa takwimu zinazoonyesha takribani watu 641 nchi nzima wamepelekwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya uhaini kutokana na vurugu za Oktoba 29 wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania.

Hatua ambayo inaibua maswali lukuki juu ya hatma za watuhumiwa hao kwenye msingi wa tuhuma nzito za makosa ya uhaini ambayo hayana dhamana na hukumu yake ikiwa ni kunyongwa hadi kufa.

Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimesema kipo tayari kuwatetea mpaka mwisho watuhumiwa 641 waliosomewa mashtaka ya uhaini na wanatarajia kuwatembelea waliopelekwa kwenye gereza la Segerea jijini la Dar es Salaam, ili kuwahoji na kufanya nao mashauriano ili kuwapa msaada wa kisheria.

Uamuzi huo wa TLS umekuja baada ya wiki hii watuhumiwa zaidi ya 600 kufikishwa katika mahakama mbalimbali nchini  wakituhumiwa kwa makossa ya uhaini.

Jeshi la polisi liliendeleza operesheni ya ‘kamatakamata’

Polisi wa kutuliza ghasia wa Tanzania wakiwatawanya waandamanaji wakati wa maandamano ya vurugu yaliyoharibu uchaguzi kufuatia kufutwa kwa wagombea wawili wakuu wa upinzani jijini Dar es Salaam, Tanzania, Oktoba 29, 2025.

Jeshi la polisi liliendeleza operesheni yake ya kuwakamata wanaodaiwa kushiriki katika vurugu za Oktoba 29 wakati wa uchaguzi Mkuu wa Tanzania.

Wakili wa TLS William Maduhu amesema, watuhumiwa wengi walioonekana mahakamani juzi walikuwa na majeraha mwilini, wengine walikuwa na alama za mijeledi migongoni na baadhi wakiwa wamebakiwa na nguo za ndani.

Hivyo TLS imejitoa kuwasaidia watuhumiwa hao kwa kuhakikisha watuhumiwa wapimwe afya zao, na ripoti za kimatibabu na afya zao ziwasilishwe mahakamani na kusisitiza kuwa iwapo serikali ina ushahidi basi TLS itawasimamia na kama hakuna ushahidi wa kutosha wa kuwakamata, basi waachiwe mara moja.

Wakati huo huo, Chama cha Mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) kimelaani vikali vurugu, mauaji, na uharibifu wa mali vilivyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025 na kimetoa pole kwa wote waliopoteza ndugu au mali.

Katika taarifa iliyotolewa na chama hicho leo, TPBA imetangaza kuunga mkono agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kufanya uchunguzi wa kina na kuwawajibisha wahusika wote kwa mujibu wa sheria.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment