Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Picha: Alina Smutko/REUTERS
Utawala wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy unakabiliwa na kashfa kubwa ya ufisadi na madai ya afisi yake kuitumia idara ya mahakama nchini humo kuwanyamazisha wakosoaji.
Kisa cha hivi majuzi kilichosababisha madai ya kuzuka kwa madai ya Zelenskiy kuitumia idara ya mahakama kama silaha ya kuwatisha wapinzani, ni kukamatwa kwa mkuu wa kampuni ya kitaifa ya nishati Ukrenergo, Volodymyr Kudrytsky, mwezi uliopita kwa madai ya ubadhirifu wa fedha.
Kudrytsky na wanaomuunga mkono wanakanusha madai hayo wakisema kukamatwa kwake kunatokana na hatua yake ya kuukosoa mkakati wa Ukraine wa kuilinda gridi ya nishati kutokana na mashambulizi ya Urusi.
Na hii leo waziri wa zamani wa nishati German Galushchenko, amesimamishwa kazi baada ya kupatikana katika uchunguzi wa mmoja wa wandani wakuu wa Zelenskiy, anayetuhumiwa kwa kuanzisha mpango wa dola milioni 100 wa kuchukua rushwa kutoka kwenye sekta ya nishati.
Galushchenko amejiondoa hatiani ila sakata hiyo imezua ghadhabu miongoni mwa Waukraine wakati ambapo gridi ya umeme ya nchi hiyo inashambuliwa na Urusi nchi hiyo ikielekea msimu wa baridi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.