Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Mshambuliaji wa kujitowa muhanga alijirupuwa karibu na gari hili na kuuwa watu 12 mjini Islamabad nchini Pakistan siku ya Jumanne (Novemba 11, 2025).Picha: Mohammad Yousuf/AP Photo/dpa/picture alliance
Mshambuliaji wa kujitowa muhanga amejiripuwa nje ya mahakama moja katika mji mkuu wa Pakistan na kuwauwa watu 12 pamoja naye mwenyewe.
Mashahidi wanaelezea kuwa mshambuliaji huyo alijiripuwa karibu na gari la polisi na kwamba mripuko huo uliwajeruhi watu wengine 27.
Kundi lililojitenga na Taliban wa Pakistan liitwalo Jamaatul Ahrar limedai kuhusika na mashambulizi hayo ya Jumanne (Novemba 11), kupitia ujumbe wa kiongozi wake, Omar Mukkaram Khurasani.
Hata hivyo, kamanda mwengine wa ngazi za juu wa kundi hilo, Sarbakaf Mohamad, alituma ujumbe wa kujitenga na mashambulizi hayo katika eneo lenye shughuli nyingi za watalii mjini Islamabad.
Waziri wa Mambo wa Ndani wa Pakistan, Mohsin Naqvi, amesema mashambulizi hayo yalifanywa na kundi la wanamgambo wa Taliban kutoka Afghanistan wanaosaidiwa na India, tuhuma ambazo hakuzithibitisha.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.