Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Waziri wa Sheria wa Ukraine, German Galushchenko, ambaye anachunguzwa sasa kwa ufisadi katika kampuni ya nyuklia ya nchi yake.Picha: Kenzo Tribouillard/AFP
Uchunguzi wa madai ya ufisadi wa kampuni ya nyuklia ya Ukraine, Energoatom, unaendelea baada ya msako mkubwa uliofanywa na vyombo vya usalama kwenye nyumba ya waziri wa zamani wa nishati, German Galushchenko.
Wizara ya sheria ya nchi hiyo iliyo kwenye vita na Urusi, ambayo kwa sasa inaongozwa na Galushchenko imethibitisha kufanyika uchunguzi huo, na kwamba mwanasiasa huyo amekubali kutoa ushirikiano kwa mamlaka za upelelezi.
Baadaye, Ofisi ya Kupambana na Ufisadi ya Ukraine (NABU) ilitowa notisi ya tuhuma dhidi ya naibu waziri mkuu wa zamani, Oleksiy Chernyshov, ambaye amekuwa akichunguzwa tangu mwezi Juni kwenye kesi nyengine inayohusiana na sekta ya ujenzi.
Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali, Serhiy Savytsky, amethibitisha notisi hiyo.
Licha ya kukabiliwa na uvamizi wa Urusi kwa miaka minne sasa, serikali ya Ukraine inayoongozwa na Rais Volodymyr Zelensky imekuwa ikishutumiwa kwa kuendekeza ufisadi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.