Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Picha: Ukrainian Presidency/Anadolu/picture alliance
Mawaziri wa nchi za kigeni wa mataifa saba yaliyoendelea kiviwanda duniani G7, wanakutana nchini Canada kwa mazungumzo yanayotarajiwa kujikita kwenye mzozo wa Ukraine.
Ripoti zinaarifu kuwa mbali na kutafuta njia ya kuumaliza mzozo huo uliodumu kwa miaka minne, huenda kukajadiliwa njia za kuyafadhili mahitaji ya Ukraine katika vita vyake na Urusi.
Mawaziri hao wanakutana wakati ambapo Rais wa marekani donald Trump aliziwekea vikwazo kampuni mbili kuu za mafuta za Urusi mwezi Oktoba akidai Rais Vladimir Putin hataki kuumaliza mzozo huo.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Italia amesema kutakuwa pia na mazungumzo kuhusu vita vya Sudan ambavyo vimesababisha mzozo mkubwa zaidi wa kiutu duniani.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.