Wairaqi wachaguwa wabunge wapya

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Mabango ya kampeni za ubunge nchini Iraq.Picha: Ismael Adnan/SOPA Images/picture alliance

Raia nchini Iraq wanapiga kura hivi leo kuchaguwa bunge jipya, kwenye uchaguzi unaofuatiliwa kwa karibu na Marekani na Iran, mahasimu wawili wenye maslahi na ushawishi mkubwa kwenye taifa hilo la Ghuba.

Iraq, ambayo imeshuhudia utulivu usio wa kawaida katika miaka ya hivi karibuni, inafanya uchaguzi wakati ikikabiliwa na hali mbaya ya miundombinu, huduma mbovu za kijamii na ufisadi uliotitia.

Taifa hilo la Kiarabu lenye wakaazi milioni 46 bado linaendelea kujijenga upya kufuatia uvamizi na ukaliaji wa Marekani na washirika wake uliopelekea kifo cha  Rais Saddam Hussein na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Zaidi ya wapigakura milioni 21 wamejiandikisha kuwachaguwa wabunge wa viti 329, vinavyowaniwa na wagombea zaidi ya 7,740. Kura imeanza kupigwa saa moja asubuhi kwa majira ya huko na vituo vitafungwa saa 12 jioni. 

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment