Mawaziri wa kigeni wa G7 wakutana juu ya Ukraine

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Viongozi wa mataifa ya G7 walipokutana mwezi Juni nchini Kanada.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa G7 wanakutana nchini Kanada kwenye mikutano inayotazamiwa kujikita kwenye mzozo wa Ukraine na Urusi na kusaka njia ya pamoja ya kukomesha vita hivyo.

Mkutano huo unaofanyika kwenye mkoa wa Nagara unaopakana na Marekani unatarajiwa kuzungumzia  ufadhili zaidi kwa Ukraine.

Mawaziri hao wanakutana baada ya Rais Donald Trump kuziwekea vikwazo kampuni mbili kubwa kabisa za mafuta za Urusi mwezi uliopita, na kumkosoa vikali Rais Vladimir Putin kwa kukataa kukomesha vita hivyo.

Trump pia ameyashinikiza mataifa ya Ulaya kuacha kununuwa mafuta ya Urusi, akidai kuwa fedha wanazotowa ndizo zinazotumiwa na Moscow kuendeleza vita vyake nchini Ukraine.

Licha ya Kiev kuendelea kukabiliwa vibaya na mashambulizi ya Moscow, Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Kanada, Anita Anand, amejizuwia kuahidi hatua zotote madhubuti kuisaidia Ukraine kwenye mazungumzo hayo ya Niagara.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment