Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Mashambulizi ya Urusi yanayolenga miundo mbinu ya nishati ya Ukraine yawaacha mamilioni ya Waukraine taabaniPicha: DW
Mamlaka nchini Ukraine zimesema mamilioni ya watu nchini humo, wameathiriwa Jumatatu kwa kukosa umeme.
Hali hiyo imejiri baada ya Urusi kushambulia miundo mbinu ya nishati mwishoni mwa wiki.
Kampuni ya taifa ya umeme nchini Ukraine Ukrenergo, imetangaza Jumatatu kuwa kutakuwa na mgao wa umeme wa saa kadhaa katika maeneo mbalimbali, kutokana na mzozo wa Urusi na Ukraine ambapo vikosi vya Urusi, vilishambulia vituo vya nishati kuelekea majira ya baridi kali.
Katika tukio jingine, shirika la Ukraine la kupambana na ufisadi limesema linafanya operesheni kubwa ya kufichua ufisadi katika sekta ya nishati ya nchi hiyo.
Shirika hilo limesema wamerekodi matukio makubwa ya uhalifu na kwamba uchunguzi huo ulishirikisha saa 1,000 za sauti zilizorekodiwa kwa kipindi cha miezi 15.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.