Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Picha: Ted Shaffrey/AP Photo/picture alliance
Rais Donald Trump amewasamehea wapambe wake walioshutumiwa kushiriki jaribio la kubatilisha ushindi wa uchaguzi wa 2020.
Kulingana na afisa mkuu wa kitengo hicho cha msamaha wa rais, Ed Martin, miongoni mwa wale ambao Donald Trump amewasamehe ni waliokuwa mawakili wake Rudy Giuliani na Sidney Powell na pia aliyekuwa afisa mwandamizi Mark Meadows ambao wamepewa msamaha bila masharti yoyote.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X, Martin amechapisha orodha ya watu 70 ambao wamesamehewa.
Majina yaliyo kwenye orodha yalihusishwa katika mpango wa kubadilisha orodha za wapiga kura katika majimbo ya ushindani mkali, yakiwemo Arizona, Georgia na Michigan, ambayo Joe Biden alikuwa amepata kura nyingi katika uchaguzi wa urais ya mwaka 2020
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.