Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Wafungwa wasiopungua 27 wamefariki gerezani nchini Ecuador katika mazingira ya kutatanisha.Picha: Luis Suarez/AFP
Wafungwa hao waligunduliwa wamekufa kwa kukosa hewa kwa sababu ya hali inayoashiria kujinyonga au kunyongwa.
Wafungwa 31 mmoja wamefariki katika gereza moja nchini Ecuador.
Hayo yamesemwa na mamlaka ya gereza SNAI, na kueleza kuwa, wafungwa 27 waliokufa waligunduliwa Jumapili jioni.
Kulingana na maafisa hao, wafungwa hao walikufa kwa kukosa hewa kwa sababu ya kujinyonga au kunyongwa. Lakini haijabainika kikamilifu matukio yaliyosababisha vifo vyao.
Awali, mamlaka hiyo iliripoti kwamba wafungwa wanne waliuawa wakati wa machafuko ndani ya gereza hilo lililoko mji wa pwani ya Ecuador, Machala. Mamlaka hiyo imesema Idara husika zimeshaanza uchunguzi kuhusu kisa hicho.
Watu wengine 34 walijeruhiwa akiwemo afisa wa polisi wakati wa machafuko hayo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.