BIASHARA YAKO INAYUMBA? HAYA NI MAKOSA 10 HATARI UNAYOFANYA…

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Wengi ambao walipuuzia mambo haya wakajikuta hawana biashara, pitia kwa umakini ili kujenga biashara yenye matokeo makubwa…

1. Huduma mbovu kwa wateja

Huduma kwa wateja ni msingi wa mafanikio ya biashara yoyote. Ukimdhulumu mteja leo, hatarudi tena kesho na atamwambia wengine wasije pia. Wateja wanahitaji kuheshimiwa, kusikilizwa, na kutatuliwa changamoto zao kwa haraka. Huduma nzuri hujenga uaminifu na uhusiano wa kudumu.

2. Bei kubwa isiyoendana na thamani

Wateja huwa wanalinganisha bei na thamani wanayoipata. Ukipandisha bei bila kutoa thamani halisi ya bidhaa au huduma, utawapoteza. Hakikisha bei zako zinaendana na ubora na zinazingatia hali ya soko.

3.Kuweka eneo lisilofaa kwa biashara.

Mahali unapoanzisha biashara ni jambo la msingi. Biashara iliyowekwa eneo lisilo na mzunguko wa watu, au lisiloeleweka kirahisi na wateja, ni sawa na kujifungia ofisi porini. Hakikisha unaweka biashara sehemu yenye upatikanaji rahisi na idadi kubwa ya watu.

4. Kutokujitangaza (Poor Marketing)

Biashara isiyojiuza haijulikani. Na usipojulikana, hupati wateja. Tumia njia mbalimbali za kutangaza kama mitandao ya kijamii, mabango, vipeperushi, promosheni na hata maongezi ya moja kwa moja. Jiweke sokoni kwa njia sahihi.

5. Kushindwa kufunga mauzo (closing sales)

Kuwa na wateja wanaoulizia bidhaa au huduma siyo mafanikio hadi wanunue. Unahitaji kuwa na ujuzi wa kuwashawishi, kujibu maswali yao, na kuwaongoza kufanya uamuzi wa kununua. Huu ni ujuzi muhimu sana unaopaswa kujifunza au kufundisha wafanyakazi wako.

6. Kutokuwa na wafanyakazi wenye sifa

Hata kama una bidhaa nzuri, ukiwa na wafanyakazi wasio na bidii, wasio na maadili ya kazi, au wasiopenda wateja, biashara itashuka. Ajiri watu sahihi, wafunze, na wahimize kufanya kazi kwa ufanisi na kwa moyo wa kuhudumia.

7. Kutokuwa na mpango wa biashara (business plan)

Biashara bila dira ni sawa na safari bila ramani. Mpango wa biashara hukusaidia kuelewa soko, kuweka malengo, kupanga bajeti, na kujua njia ya kuyafikia mafanikio. Bila mpango, ni rahisi kupotea na kufanya maamuzi ya kihisia.

8. Mwonekano mbaya wa ofisi yako.

Wateja wengi huvutiwa na mwonekano wa biashara yako. Jitahidi kuboresha mazingira, usafi, tengeneza maudhui zenye ushawishi na kuvutia wateja wako.

9. Kuendesha biashara kiujanja badala ya kitaalamu.

Biashara nyingi hufa kwa sababu wamiliki wake wanaendesha kwa mazoea au ujanja badala ya taaluma. Ni muhimu kujifunza, kusoma vitabu, kuhudhuria semina, au kupata ushauri wa kitaalamu ili biashara yako iwe ya kisasa na endelevu.

10. Kutokuwa na uvumilivu na nidhamu

Mafanikio hayaji haraka. Wamiliki wengi huacha biashara mapema kabla haijakomaa. Inahitaji subira, nidhamu ya kifedha, kujifunza kutoka kwa makosa, na kuendelea kuboresha kila siku. Nidhamu ni nguzo ya kila mafanikio.

Ni jambo gani limekuwa likikusumbua bila mafanikio yoyote. Niandikie kwenye comment hapa chini ili niweze kukusaidia haraka sana

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment