Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Zaidi ya safari za ndege 1,400 kwenda, kutoka, au ndani ya Marekani zilifutwa Jumamosi baada ya mashirika ya ndege kuambiwa wiki hii kupunguza safari za anga wakati wa kufungwa kwa serikali ya nchi hiyo.
Karibu safari za ndege 6,000 pia ziliahirishwa, kutoka zaidi ya safari za ndege 7,000 siku ya Ijumaa, kulingana na FlightAware inayofuatilia safari za ngege.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga, (FAA) ilitangaza mapema wiki hiyo kwamba itapunguza shughuli za safiri za anga kwa hadi 10% katika viwanja 40 vya ndege vyenye shughuli nyingi zaidi nchini humo, huku wadhibiti wa safari za anga, ambao wanafanya kazi bila malipo wakati wa kufungwa, wakiripoti uchovu.
Warepublican na Wademokrat wanabaki kugawanyika kuhusu jinsi ya kumaliza mkwamo katika Bunge huku kufungwa kwa serikali, ambako kulianza Oktoba 1, kukiendelea.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.