Mamia wahamishwa Ufilipino kabla ya kimbunga Fung-wong kutua

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

.

Zaidi ya watu 900,000 wamehamishwa nchini Ufilipino kabla ya kimbunga Fung-wong kutua Jumapili jioni.

Kimbunga hicho kinasafiri kwa kilomita 185 kwa saa (115mph) kikiandamana na upepo unaovuma kwa kasi ya 230km/h (143mph), kulingana na mamlaka ya hali ya hewa nchini.

Eneo la mashariki la Bicol lilikuwa sehemu ya kwanza ya Ufilipino kuathiriwa moja kwa moja na dhoruba hiyo Jumapili asubuhi, huku Luzon likitarajiwa kukumbwa na kimbunga hicho Jumapili usiku.

Kimbunga Fung-wong – ambacho kinajulikana kama Uwan huko Ufilipino – kinatua siku chache baada ya dhoruba ya awali, Kalmaegi, vifo vya watu 200 na kusababisha uharibifu mkubwa.

Shule kadhaa zimesitisha masomo siku ya Jumatatu au kuzihamisha mtandaoni, huku takriban safari 300 za ndege zikiahirishawa.

Fung-wong inatarajiwa kupunguza makali yake baada ya kutua katika wilaya za Baler na Casiguran, lakini kuna uwezekano wa dhoruba hiyokugeuka kimbunga itakapoelekea Luzon.

Zaidi ya 200mm ya mvua inatarajiwa kunyesha katika maeneo ya Luzon, na kati ya mm 100 hadi mm200 mjini Manilla.

Mvua hiyo inatarajiwa kusababisha mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment