Watu 98 washtakiwa kwa uhaini nchini Tanzania

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Maandamano ya wakati wa uchaguzi nchini Tanzania mnamo Oktoba 29, 2025Picha: AP Photo/picture alliance

Waendesha mashtaka nchini Tanzania wamewashtaki watu 98 kwa uhaini kwa madai ya kuhusika katika maandamano ya ghasia yaliyozuka wakati wa uchaguzi mkuu wiki iliyopita.

Nyaraka hizo katika mahakama ya hakimu mkaazi Dar es Salaam, zimesema kuwa washtakiwa walikuwa na nia ya kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025 kwa madhumuni ya kuitisha mamlaka ya nchi hiyo na kusababisha uharibifu wa mali za serikali.

Hata hivyo, hakukuwa na ufafanuzi wa tuhuma maalum dhidi ya washtakiwa hao isipokuwa kwa mfanyabiashara mmoja mwanamke ambaye ameshtumiwa kwa kuwahimiza watu kununua barakoa za kujikinga na gesi za machozi kutoka kwa biashara yake wakati wa maandamano hayo.

Rais wa chama kikuu cha wanasheria nchini Tanzania, Boniface Mwabukusi, amesema hadhani kama washtakiwa hao waliwakilishwa na wakili.

Serikali haijajibu ombi la tamko kuhusu hali hiyo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment