Pezeshkian: Iran inatafuta amani lakini haitoshurutishwa

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Rais wa Iran, Masoud PezeshkianPicha: Iranian Presidency/Anadolu/picture alliance

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema kuwa Iran inatafuta amani, lakini haitashurutishwa wala kuacha mpango wake wa nyuklia. Haya yameripotiwa leo na vyombo vya habari vya serikali.

Akizungumza jana katika Ikulu ya White House alipoandaa dhifa rasmi ya jioni kwa kikundi cha C5 +1 ambacho kinajumuisha jamhuri tano za Asia ya Kati Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan, Turkmenistan, na Uzbekistan, Rais wa Marekani Donald Trump alisema  Iran imekuwa ikiuliza ikiwa vikwazo hivyo vinaweza kuondolewa.

Trump ameongeza kusema kuwa Iran ina vikwazo vikubwa sana vya Marekani na inafanya kuwa vigumu kwa nchi hiyo kufanya kile ambacho  ingependa kufanya.

Hata hivyo amesema yuko tayari kusikiza hilo na kuona kitakachotokea.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment