Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Ulaya, Kaja KallasPicha: Nicolas Tucat/AFP
Nchi za Umoja wa Ulaya hazitatoa tena viza za kuingia zaidi ya mara moja katika mataifa ya Umoja huo kwa raia wa Urusi, kufuatia “vitendo vya hujuma na uwezekano wa matumizi mabaya” ya viza hizo.
Halmashauri ya Umoja wa Ulaya imesema raia wa Urusi watalazimika kuomba viza mpya kila wanapotaka kuingia Ulaya kwa lengo la kuwachunguza mara kwa mara waombaji wa viza hizo ili kupunguza uwezekano wa hatari.
Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine wajenga mazingira hatari
Katika taarifa, mjumbe maalumu wa Umoja huo Kaja Kallas, amesema kwa miongo kadhaa, uvamizi haramu wa Urusi dhidi ya Ukraine umejenga mazingira hatari zaidi ya usalama Ulaya.
Pia amesema kwa sasa wanakabiliwa na usumbufu wa droni na hujuma kwenye ardhi yao kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.
Kallas pia amesema ni jukumu la Umoja huo wa Ulaya kuwalinda raia wao.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.