Trump atarajia kikosi cha kimataifa cha kuleta utulivu Gaza

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Rais wa Marekani, Donald TrumpPicha: Chandan Khanna/AFP

Rais wa Marekani Donald Trump amesema anatarajia kuwa hivi karibuni, kikosi cha kimataifa cha kuleta utulivu kinachoratibiwa na Marekani kitawasili Ukanda wa Gaza.

Wakati wa hafla katika Ikulu ya White House akiwa na viongozi wa Asia ya Kati, Trump alisema kikosi kazi hicho cha kimataifa cha baada ya vita ambacho kinatarajiwa kutumwa Gaza kina uwezekano mkubwa kujumuisha wanajeshi kutoka Misri, Qatar, Uturuki na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Pia amesema kuna nchi nyingi ambazo zimejitolea na kujituma kushughulikia matatizo mbali mbali katika ukanda wa Gaza.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment