Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Siku moja baada ya mashambulizi makali ya Israel katika maeneo ya Lebanon, Wizara ya Mambo ya kigeni ya Iran iliita hatua hiyo “mashambulizi ya kihalifu” ambayo “yalibuniwa na kutekelezwa kwa uungaji mkono kamili na ushirikiano wa Marekani.”
Israel ilishambulia kwa mabomu maeneo ya kusini mwa Lebanon mnamo Alhamisi, Novemba 6, katika moja ya mashambulizi yake mazito zaidi dhidi ya Lebanon tangu kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano mwaka jana.
Jeshi la Israel hapo awali lilikuwa limetoa onyo la kuhama kwa wakazi katika miji na vijiji kadhaa.
Israel inasema mashambulizi yake yamelenga maeneo ya kijeshi ya Hezbollah na miundombinu nchini Lebanon.
Hata hivyo,Hezbollah inasema raia wamejeruhiwa na maeneo ya makazi kuharibiwa katika mashambulizi haya.
Sasa, kutokana na mzozo huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetoa taarifa ikitaka Umoja wa Mataifa, jumuiya ya kimataifa na nchi za ukanda huo zichukue hatua za kukabiliana na sera za kichochezi za Israel.
China yazindua chombo kipya cha kubeba ndege katika ushindani wa kiteknolojia na Marekani

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya China, meli hiyo iliyoundwa kwa teknolojia ya juu zaidi ya kubeba ndege nchini humo, Fujian, kimekabidhiwa rasmi kwa jeshi la nchi hiyo.
Meli hiyo ilizinduliwa siku chache zilizopita katika hafla kubwa iliyohudhuriwa na Rais Xi Jinping wa China.
Fujian, meli ya tatu kwa ukubwa inayotumika kubeba ndege nchini China, ikitumia umeme huruhusu ndege kuruka kwa kasi zaidi.
Kuzinduliwa kwa meli hii ni hatua muhimu kwa Beijing, kufuatia China sasa kuwa na jeshi kubwa zaidi la wanamaji duniani kwa kigezo cha idadi ya meli.
Chini ya uongozi wa Xi Jinping, China inaimarisha jeshi lake la majini kwa kasi, na kuendeleza shinikizo kwa Marekani na washirika wake.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali, Fujian inaweza kuhudumia aina tatu tofauti za ndege kwa kutumia teknolojia ya umeme.
Chombo hicho, ambacho kinazalishwa nchini China, kinaweza kubeba ndege zenye silaha nzito zaidi na mafuta mengi zaidi, kushambulia adui kutoka umbali mkubwa zaidi, kipengele ambacho kinaifanya kuwa na nguvu zaidi kuliko ndege mbili za awali za nchi hiyo, Liaoning na Shandong zilizotengenezwa Urusi.
Vyombo vya habari vya serikali ya China viliipongeza Fujian kwa “hatua muhimu” katika maendeleo ya jeshi la wanamaji la nchi hiyo.
Ruto amtaka Zelensky kuwaachilia Wakenya wanaoshikiliwa Ukraine

Rais wa Kenya amemtaka rais wa Ukraine Volodmir Zelensky kuwaachilia Wakenya waliotekwa nchini Ukraine ambao waliandikishwa kinyume cha sheria kupigana vita vinavyoendelea dhidi ya Urusi.
Rais wa Kenya William Ruto alisema alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambapo wote wawili “walielezea wasiwasi wao kwamba vijana wa Kenya walikuwa wakisajiliwa kupigana vita nchini Ukraine kinyume cha sheria.”
Kupitia chapisho lake katika mtandao wa X rais Ruto hajabainisha ni nani aliyewasajili licha ya kueleza kwamba alikuwa amewasiliana na Zelensky “kuhusu ombi la kuwezesha kuachiliwa kwa Wakenya wote waliokuwa nchini Ukraine,” na kiongozi huyo wa Ukraine “alipokea vema suala hili.
Kwa upande wake Volodymyr Zelensky pia aliripoti mazungumzo baina yake ya rais Ruto.
Alisema walijadili “maswala ya Urusi kusajili raia wa kigeni kushiriki katika vita.” Rais wa Ukraine aliahidi “kushughulikia na kukomesha hili.”
Wiki hii, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alisema kuwa Waafrika Kusini wanaopigana nchini Ukraine wamenaswa huko Donbas.
RSF iheshimu usitishwaji mapigano Sudan

Serikali ya Sudan inasema itahitaji hakikisho kutoka kwa jumuiya ya kimataifa kwamba RSF itaheshimu pendekezo la hivi karibuni la kusitisha mapigano kabla ya kukubaliana nalo.
Haya yanajiri huku kukiripotiwa ripoti za mashambulizi ya ndege zisizo na rubani katika mji mkuu Khartoum, saa chache tu baada ya kundi la wanamgambo kukiri kuwa limekubali usitishaji mapigano uliosimamiwa na Marekani.
Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Pretoria, balozi wa Sudan nchini Afrika Kusini alisema ni mapema mno kwa nchi yake kujibu pendekezo la Marekani la kusitisha mapigano.
Balozi Osman Mohammed aliambia BBC kwamba usitishaji mapigano hapo awali haukuheshimiwa na Rapid Support Forces (RSF).
Alisema RSF imetumia mapatano hayo kupata mafanikio ya kimaeneo na kushambulia vikosi vya serikali.
Kwa mujibu wa Balozi Mohammed, uongozi wa RSF hauna udhibiti kamili wa wanajeshi wake, wakiwemo mamluki wa kigeni wanaowatumikia.
Alisema kuwa nchi yake itahitaji dhamana kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na UAE ambayo imekuwa ikishutumiwa kuunga mkono RSF.
Wakati huo huo nchini Sudan kumeripotiwa milipuko katika mji mkuu Khartoum, na pia katika mji wa Atbara katika Jimbo la Mto Nile.
Miji yote miwili iko chini ya udhibiti wa Wanajeshi wa Sudan.
Hofu ya machafuko mapya yaikumba Ethiopia

Afisa mwandamizi wa Tigray kaskazini mwa Ethiopia ameiambia BBC kwamba serikali kuu imezindua mashambulizi ya ndege isiyokuwa na rubani dhidi ya waasi wa zamani wakati huu hofu ya kuibuka kwa machafuko mapya ikiongezeka katika eneo hilo.
Hatua hii inakuja siku moja baada ya vikosi vya Tigray vikituhumiwa kwa kuvamia jimbo Jirani na kudhibiti vijiji sita.
Hatua hii inaripotiwa kwa mara ya kwanza kati ya serikali na vikosi vya Tigray tangu kutamatika kwa moja ya mgogoro mbaya zaidi katika ukanda huu kwa makubaliano ya amani iliyofikiwa takriban miaka mitatu iliyopita.
Akizungumza na BBC afisa Mwandamizi wa jeshi la Tigray amesema shambulizi la ndege isiyokuwa na rubani ilisabbaisha madhara kwa kiwango kidogo.
Hata hivyo hakuna kauli yoyote iliyotolewa na serikali na BBC haijathibitisha shambulizi hilo.
Mnamo Alhamisi maafisa kutoka Afar,mji Jirani na Trigray alivishutumu vikosi vya Tigray kwa kutekeleza shambulizi na kukiuka makubalino ya amani.
Mamia kwa maelfu ya watu walikadiriwa kupoteza maisha katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka miwili.
Waangalizi wanaonya kwamba mgogoro unaweza kuzuka upya katika eneo hilo.
17 wafariki dunia wakiwa gerezani ndani ya mwaka mmoja nchini Kenya- ripoti

Zaidi ya watu 100,000 waliingia katika mitaa ya mji mkuu, Nairobi, tarehe 25 Juni 2024 kuwashinikiza Wabunge kutopitisha mswada tata wa fedha.
Shirika la kutetea haki za kibinadamu la IMLU limesema wakenya 17 wameuawa kwenye seli za polisi huku visa hivyo vikichunguzwa mwaka huu pekee.
“Kenya inashuhudia ongezeko la vifo vinavyotokea wakiwa gerezani kati ya 2024 na 2025, hali inayotia wasiwasi mkubwa,” amesema Wangechi Grace Kahuria, Mkurugenzi mkuu wa IMLU.
Ripoti hiyo ya IMLU pia imeisema watu wengine 59 waliuawa na polisi kwenye visa vya utumizi wa nguvu kupita kiasi.
”Kile tumeona nchini Kenya kiwango cha kunakili visa vya mauaji haya hakikidhi kanuni za kimataifa” asema Profesa Dkt. Djordje Alempijevic, mjumbe wa UN.
Vifo hivi viliripotiwa katika vituo vya polisi na rumande, katika angalau kaunti 10, zikiwemo Nairobi, Nakuru, Murang’a, Siaya, Mombasa, Kakamega na Busia.
Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa kulikuwa na jitihada za kuficha sababu za baadhi ya vifo hivi, huku familia nyingi bado zikisubiri haki.
Sababu za vifo ni tofauti, zikiwemo:
• Kupungua kwa nguvu za moyo na mapafu (cardiorespiratory failure) • Kupungua kwa nguvu za moyo kutokana na majeraha mengi (cardiogenic shock)
”Hali hii inaashiria matukio mbalimbali yakiwemo mashambulizi ya kimwili, kuteswa, na kufungwa hewani, huku baadhi ya visa vikionyesha ujaribu wa kuonesha kuwa mtu alijitoa uhai.” anaongezea Mkurugenzi mkuu wa IMLU.
Visa hivi vinaripotiwa licha ya kuwepo kwa Sheria ya Huduma za Kitaifa ya Corona inayolazimisha kuanzishwa kwa shirika huru kuchunguza vifo visivyoeleweka; lakini utekelezaji wake umekwamishwa.
Hali hii inatokea huku bunge la Seneti ya Kenya ikijadili mswada wa kuweka kamera za siri za CCTV katika vituo vya polisi, hatua inayolenga kupunguza vifo gerezani na matumizi makali ya nguvu za polisi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.