Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Mkuu wa jeshi la Ujerumani, Carsten BreuerPicha: Sean Gallup/Getty Images
Mkuu wa jeshi la Ujerumani Carsten Breuer, ameonya leo kuwa Urusi haipaswi kabisa kufikiria kwamba inaweza kushinda vita dhidi ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO au hata dhidi ya mwanachama yeyote wa muungano huo wa kijeshi.
Breuer ametoa onyo hilo wakati wa hotuba yake kwa viongozi wakuu wa kijeshi nchini humo.
Breuer amesema wanahitaji kuyaangazia kwa undani mafunzo waliyoyapata kutokana na vita nchini Ukraine, kuyatumia kwa maslahi yao na kuunda mifumo inayofaa kwa sababu vita nchini Ukraine ndio mfano wao.
Pia amesema Urusi ilitarajia ushindi wa haraka ilipoivamia Ukraine mnamo mwaka 2022.
Mkuu huyo ameongeza kuwa lazima waizuie Urusi kutofanya kosa lingine kama hilo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.