Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Mark Rutte, Katibu Mkuu wa jumuiya ya kujihami NATO atapokea tuzo ya amani ya WestphaliaPicha: Nicolas Tucat/AFP/Getty Images
Jumuiya ya kujihami ya NATO itapokea Tuzo ya Kimataifa ya Amani ya Westphalia ya mwaka 2026. Tuzo hiyo itatolewa katika mji wa Münster.
Jumuiya ya kujihami ya NATO itapokea Tuzo ya Kimataifa ya Amani ya Westphalia ya mwaka 2026.
Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte atakubali na kuipokea tuzo hiyo kwa niaba ya muungano huo wa kijeshi katika ukumbi wa mji wa Münster, kwa mujibu wa tangazo lililotolewa jana Jumatano na waandaaji katika jiji hilo la magharibi mwa Ujerumani.
Msingi wa tuzo hiyo unahusiana na mikataba miwili ya amani iliyosainiwa mnamo 1648 ambayo ilifikisha mwisho mfululizo wa vita Ulaya ya Kati kati ya 1618 na 1648.
Washindi wa zamani wa tuzo hiyo, ambayo hutolewa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Westfalia na Lippe (WWL) kila baada ya miaka miwili, ni pamoja na makansela wa zamani wa Ujerumani Helmut Kohl na Helmut Schmidt, wafanyakazi wa Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS), Mfalme Abdullah II wa Jordan na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.