Mkutano wa awali kabla ya COP30 wafanyika Brazil

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Mkutano wa kilele wa mabadiliko ya tabianchi kwa mwaka 2030 kufanyika Belem, BrazilPicha: Lucio Tavora/Xinhua/IMAGO

Viongozi wa mataifa mbalimbali duniani wanakutana Alhamisi 06.11.2025 huko Belem, Brazil katika juhudi za kuendelea kutoa kipaumbele kwa janga la athari za mabadiliko ya tabianchi.

Mkutano huo unafanyika siku chache kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP30 utakaonza wiki ijayo.

Miongoni mwa viongozi watakaohuduria ni Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. Katika mkutano huo karibu kila taifa litashiriki japo Marekani haitakuwa na mwakilishi yoyote.

Juhudi zaidi zatakiwa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi

Viongozi wa dunia wameendelea kulaumiwa kwa kusuasua katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Mapema Jumatano, wanaharakati wa mashirika kadhaa walifanya maandamano katika mji wa Belem kunakofanyika mkutano huo wakishinikiza hatua zaidi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment