Marekani yatishia kutokuunga mkono ujumbe wa amani wa Abyei

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph |RFA

Vikosi vya kulinda amani kutoka Ethiopia ni sehemu ya tume ya amani ya Umoja wa Mataifa (UNISFA) huko AbyeiPicha: Albert Gonzales Farran/AFP/Getty Images

Marekani imesema itaondoa uungwaji wake mkono wa kurefusha ujumbe wa amani wa kimataifa katika eneo linalozozaniwa la Abyei kati ya Sudan na Sudan Kusini.

Marekani imetishia kupinga kurejeshwa kwa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Abyei, eneo lenye mzozo kati ya Sudan iliyokumbwa na vita na Sudan Kusini, mpaka pande zote mbili zitakapoyakubali makubaliano ya amani ya 2011.

Katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika jana Jumatano, balozi wa Marekani katika umoja huo Mike Waltz alianisha masharti ya Marekani ya kurefusha kwa mamlaka ya  kikosi maalumu cha Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Abyei (UNISFA), ambayo yanafika mwisho Novemba 15.

Waltz aliliambia Baraza la Usalama kwamba Sudan na Sudan Kusini lazima sasa zitekeleze ahadi zao kwa makubaliano ya amani ya 2011 na mamlaka ya UNISFA ili kupata uungwaji mkono wa Marekani kwa urerushaji wa mamlaka ya kikosi hicho.

Waltz alisema pia nchi hizo jirani zinahitaji kuhakikisha kwamba Abyei ni eneo lisilo na wanajeshi, kuanzisha mipango ya muda ya kiutawala na usalama kama vile kikosi cha pamoja cha polisi cha Abyei, na kubaini hadhi ya mwisho ya eneo hilo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment