Upinzani Tanzania wadai kutupwa kisiri maiti za waandamanaji

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Maafisa wa polisi wakiburuta maiti ya mwandamanaji aliyeuawa katika mpaka wa Namanga, TanzaniaPicha: Thomas Mukoya/REUTERS

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA chadai kuwa vikosi vya usalama vilikuwa vikitupa miili ya mamia ya waliouawa katika ghasia za uchaguzi.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema Brenda Rupia akizungumza kwa njia ya simu kutoka Dar es Salaam, amesema mioyo ya Watanzania inavuja damu hivi sasa, kwasababu hilo ni jambo jipya kwao.

Lori za jeshi zaripotiwa kubeba maiti za waandamanaji

Ofisa mwingine wa Chadema, Deogratius Munishi, amesema alipokea ujumbe jana kutoka kwa raia karibu na mji wa Arusha ambao waliripoti kuona lori mbili za jeshi zikitoka kwenye eneo la vyumba vya kuhifadhia maiti zikiwa zimejazwa miili ya waliouawa.

”Siku chache zilizopita tulisikia taarifa kuwa polisi wanakwenda katika hospitali mbalimbali kuchukua maiti za waliouawa wakati wa maandamano na tunasikia baadhi yao wanazikwa kwenye makaburi ya pamoja, kwa hiyo, haya ndiyo mambo ambayo tunataka vyombo vya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa vije kuyathibitisha.”Mashirika ya haki na wadau mbali mbali wamelaani mauaji hayo nchini Tanzania.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment