Muhimu: Mambo Ya Kuzingatia Mteja Anapofika Kwenye Biashara Yako.

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Mteja anapofika kwenye biashara yako ni jambo la msingi kukuza biashara yako. Kwa kufuata mambo haya utapata matokeo makubwa.

1. Mpokee kwa ukarimu


Simama na mpokee kwa tabasamu huku ukiwa na furaha. Mpe salamu na neno la karibu sana kwenye biashara/ofisi yako.
Ukarimu wa mwanzo hujenga picha chanya ya huduma zako.

2. Msikilize kwa umakini


Toa muda na umakini wako wote, acha simu au shughuli nyingine ulizokuwa unafanya.

Msikilize ili kuelewa changamoto au hitaji lake kikamilifu. Mteja anajisikia kusikilizwa, na atakuwa tayari kueleza shida yake vizuri zaidi.

3. Mpe suluhisho la changamoto yake


Baada ya kuelewa hitaji lake, toa suluhisho sahihi kwa haraka na kwa weledi.

Mpe usaidizi kama unachagua bidhaa, na mpe uchaguzi kulingana na uhitaji wake.
Na hakikisha unampatia huduma au bidhaa bora itakayoondoa changamoto yake.

Jali muda wake kwa kutoa huduma yenye ufanisi bila kupoteza wakati. Wateja wengi wanajali muda wao

4. Mshukuru na jenga uhusiano


Usimwache mteja aondoke bila kushukuru.
Mwambie: “Asante kwa kuchagua huduma/bidhaa zetu, karibu tena.

Kumbuka ameacha maduka mengi na kukuchagua wewe, hivyo thamini uamuzi wake.

Chukua mawasiliano yake ili kuendelea kumsaidia na kufuatilia maendeleo yake baada ya huduma au bidhaa.

Ukifanya vitu hivi utapata wateja wa kudumu na wataendelea kuwa sehemu ya biashara yako.

Sasa naomba uniambie unahitaji usaidizi katika jambo gani hapa.

Niandikie kwenye comment ili tuweze kujadili kwa kina na nikusaidie zaidi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment