IAEA: Iran inapaswa kuimarisha ushirikiano kuhusu nyuklia

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Mkuu wa Shirika la IAEA Rafael GrossiPicha: Helmut Fohringer/APA/picture alliance

Iran lazima iimarishe ushirikiano wake na wakaguzi wa Umoja wa Mataifa ili kuepuka kuzidisha mvutano na nchi za Magharibi.Haya yameripotiwa na gazeti la Financial Times lililomnukuu mkuu wa Shirika la IAEA Rafael Grossi.

Grossi ameliambia gazeti hilo  kwamba wakati shirika la IAEA likiwa tayari limefanya duru kadhaa za ukaguzi nchini Iran tangu uhasama na Israel mnamo mwezi Juni, halijaruhusiwa kufikia vinuu vya nyuklia kama vile Fordow, Natanz na Isfahan, ambazo zilishambuliwa na Marekani .

Iran yapaswa kuzingatia yaliomo katika makubaliano ya nyuklia

Grossi pia amesema wakati shirika hilo linajaribu kushirikiana na Iran kwa maelewano, nchi hiyo bado inahitajika kuzingatia yaliomo.

Kwa upande wake, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Esmaeil Baghaei, amesema Grossi anafahamu kikamilifu hali ya amani ya mpango wa nyuklia wa Iran na hapaswi kutoa maoni aliyoyataja kutokuwa na msingi juu yake.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment