EU bado haijafikia makubaliano ya malengo ya hali ya hewa

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Bendera za Umoja wa UlayaPicha: Virginia Mayo/AP Photo/picture alliance

Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya bado hazijafikia makubaliano kuhusu malengo muhimu ya uzalishaji wa hewa chafuzi kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa wa COP30 utakaofanyika wiki ijayo nchini Brazil.

Maafisa wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels wamesema mazungumzo yaliofanyika jana Jumanne mjini humo yalimalizika bila maelewano na kuendelea usiku kucha.

Mapema leo, msemaji wa Denmark ambayo kwasasa inashikilia urais wa zamu, amesema wanaamini kuwa wana msingi wa makubaliano ya kisiasa.

Pia amesema wanatarajia kuhitimisha rasmi makubaliano watakaporejea kukutana tena baada ya saa chache.

EU yasisitiza kuhusu umuhimu wa mazungumzo ya hali ya hewa

Maafisa wa Umoja wa Ulaya wamesisitiza umuhimu wa mazungumzo hayo, ambayo yanakuja kabla ya mkutano huo wa Brazil.

Waziri wa mazingira wa Ufaransa Monique Barbut ameonya kwamba kuhudhuria mkutano huo bila makubaliano yoyote, kutasababisha kile alichokiita janga kwa Umoja wa Ulaya.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment