ENEO TAJIRI SANA NI MAKABURINI.

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Mtu mmoja aliwahi kusema, “Sehemu tajiri zaidi duniani si kwenye machimbo ya madini au maeneo yenye mafuta, bali ni kwenye makaburi.”

Hii ni kwa sababu watu wengi wanakufa wakiwa na mipango, malengo, na vipaji ambavyo hawakuwahi kuonesha kwenye jamii.

Inawezekana nawe unasoma ujumbe huu huku ukiwa na wazo la biashara, una kipaji, au malengo ambayo bado hujaanza kuyafanyia kazi. Kumbuka, dunia haitajua uwezo wako hadi pale utakapo onesha. Ulimwengu upo tayari kupokea chapa yako, jina lako, na alama unayotaka kuacha.

Amua leo, kwa makusudi ya dhati, kuonesha kipaji chako. Ikiwa ni biashara uliyokuwa umeipanga, anza leo hata kwa hatua ndogo. Hatua hiyo itakupa hamasa ya kuendelea na hatimaye kufanikisha ndoto zako.

Wewe ni mshindi chukua hatua na uishi ndoto zako.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment