Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamelaani matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025.
THRC na TLS wametaja matukio kama mauaji, mateso, ukamataji holela wa raia yanaashiria ukiukaji wa haki za binadamu.
Katika taarifa yao ya pamoja waliyoitoa leo Novemba 4, 2025, na kusainiwa na Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa, na Rais wa TLS Boniface Mwabukusi inasikitishwa na mauaji ya vijana wengi wakati wa maandamano ya amani hasa katika maeneo yasiyo ya maandamano.
Taasisi hizo zimeacha alama mbaya katika historia ya haki, demokrasia, na utawala wa sheria nchini, na kutaka uchunguzi huru na kuwawajibisha wote waliohusika. Tayari Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ambayo ni idara huru ya Serikali, imesema inaanza uchunguzi wa kina, na kutoa majibu ndani ya miezi miwili.
“Wazazi wengine ambao hawakuona miili ya watoto wao wameanza kuulizia watapataje miili hiyo ili wakawazike. Ni muhimu sana wazazi wakapewa miili ya vijana wao walioumia au kufariki,” Inasema sehemu ya taarifa hiyo.
Taasisi hizo za THRDC na TLS zimekemea kuhusu uharibifu wa mali za umma na binafsi na kusisitiza mazungumzo zaidi kuliko matumizi ya nguvu.
Imetaja pia kuzimwa kwa mitandao kuanzia Oktoba 29 hadi Novemba 3 ni ukiukaji mwingine wa haki ya kupata taarifa na mawasiliano.
Akizungumza baada ya kuapishwa mwishoni mwa wiki, Rais Samia Suluhu alitoa onyo kwa waliohamasisha maandamano na kufanya uvunjivu wa amani, ikiwmeo pia kuharibu mali za umma na binafsi.
Maandamano hayo yalianza siku ya uchaguzi Jumatano iliyopita, ambapo baadhi ya waandamanaji walichana mabango ya Rais Samia na kuchoma majengo ya serikali. Polisi na vyombo vingine vya dola vilitumika kukabiliana na waandamanaji. Wengi wa waandamanaji walikuwa wakilalamikia kutoshiriki kwa wagombea wawili wakuu wa upinzani, Tundu Lissu na Luhaga Mpina.
Lissu na chama chake cha CHADEMA, chama kikuu cha upinzani kilijiondoa katika kinyang’anyiro hicho, kikidai kufanyika kwa mabadiliko ya sheria za uchaguzi kabla ya uchaguzi mwingine wowote, huku Mpina wa ACT Wazalendo aliondolewa na INEC kwa madai ya kutokidhi vigezo vya kisheria.
Dereva awagonga watembea kwa miguu Ufaransa, tisa wajeruhiwa

Dereva amewavamia watembea kwa miguu na waendesha baiskeli katika kisiwa cha Oleron cha Ufaransa karibu na pwani ya Atlantiki siku ya Jumatano, Waziri wa Mambo ya Ndani Laurent Nunez alisema, na takriban watu tisa walijeruhiwa kabla ya dereva huyo kukamatwa, kulingana na maafisa wa eneo hilo.
Mshukiwa mwenye umri wa miaka 35 alipaza sauti akisema “Allahu Akbar” ikimaanisha (“Mungu ni Mkuu”) alipokamatwa na polisi, mwendesha mashtaka wa eneo hilo, Arnaud Laraize, aliliambia gazeti la Sud Ouest.
Mbunge wa eneo hilo Olivier Falorni, hata hivyo, alisema sababu ya shambulio hilo kwenye kisiwa tulivu kinachopendwa na watalii wakati wa kiangazi bado haijajulikana, akisema mshukiwa hakuwa kwenye orodha ya Ufaransa ya watu wenye itikadi kali.
Vyombo vya habari vya Ufaransa vilisema ofisi ya mwendesha mashitaka wa kupambana na ugaidi haikuwa inasimamia uchunguzi huo katika hatua hii, na kwamba uchunguzi wa jaribio la mauaji kwa sasa unashughulikiwa na ofisi ya mwendesha mashtaka wa eneo la La Rochelle.
Ofisi ya mwendesha mashtaka dhidi ya ugaidi haikuweza kupatikana mara moja ili kutoa maoni yake.
Takriban watu tisa walijeruhiwa wakati gari la mshukiwa lilipowagonga katika maeneo mbalimbali ya kisiwa cha Oleron, meya wa Dolus-d’Oleron, Thibault Brechkoff, aliiambia BFM TV.
Nunez alisema wawili kati ya waliojeruhiwa walikuwa katika uangalizi maalum – baadhi ya vyombo vya habari vya Ufaransa baadaye vilisema hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa wanne kati yao.
Gazeti la Le Parisien lilisema wachunguzi wanaangalia uwezekano kwamba mshukiwa anaweza kuwa na matatizo ya kiakili.
Tume ya Haki za Binadamu Tanzania kuchunguza maandamano ya uchaguzi

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Nchini Tanzania (THBUB) imesema itaanzisha uchunguzi wa kina kufuatia maandamano yalioshuhudiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025, na kusababisha uharibifu wa mali na vifo vya raia.
Ingawa Tume hiyo inasema kuwa bado haifahamu ukubwa wa tatizo, lakini inaisitiza kwamba matokeo ya uchunguzi huo yanaweza kukamilika chini ya miezi miwili.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni idara huru ya Serikali, iliyoanzishwa kama taasisi ya Kitaifa iliyo kitovu cha kukuza na kulinda haki za binadamu na utawala bora nchini Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano, Novemba 5, 2025 jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu, anasema matokeo ya uchunguzi huo ndio itaamua namna ya kuishauri Serikali ili kuepuka vurugu katika chaguzi zingine zijazo.
“Matukio ya aina hiyo hayawezi kuvumiliwa katika jamii inayothamini amani na utawala wa sheria” Alisema na kuongeza “kwa namna yoyote ile, matukio ya aina hii yaliyotokea hayapaswi kuungwa mkono, kwa sababu yanavunja amani ya nchi na kuhatarisha usalama wa wananchi,”.
“Sisi kama Tume, kutokana na matukio hayo, tumeamua kufanya uchunguzi wa kina na tayari tumejipanga vizuri kuhakikisha jambo hili linashughulikiwa ipasavyo”, anasema Mwaimu.
Maandamano hayo yalianza siku ya uchaguzi Jumatano iliyopita, ambapo baadhi ya waandamanaji walichana mabango ya Rais Samia na kuchoma majengo ya serikali.
Polisi na vyombo vingine vya dola vilitumika kukabiliana na waandamanaji.
Urusi inasema inawaondoa wanajeshi wa Ukraine huko Pokrovsk

Urusi imesema Jumatano kwamba vikosi vyake vilikuwa vinasonga mbele kaskazini ndani ya mji wa Pokrovsk wa Ukraine na kuwaondoa wanajeshi wa Kyiv katika harakati za kuchukua udhibiti kamili wa kile ambacho kimekuwa kitovu muhimu cha usafirishaji kwa jeshi la Ukraine.
Ukraine imekiri kuwa wanajeshi wake wanakabiliwa na wakati mgumu katika mji huo wa kimkakati wa mashariki, ambao Urusi imekuwa ikijaribu kuuteka kwa zaidi ya mwaka mmoja, lakini inakanusha kuwa wamezingirwa na kusema kwamba wanaendelea kuijiimarisha.
Urusi inachukulia mji huo kama fursa ya kuweza kuteka asilimia 10 iliyosalia, au kilomita za mraba 5,000 (maili za mraba 1,930) za eneo la mashariki la viwanda la Donbas la Ukraine, mojawapo ya malengo yake kuu katika vita vilivyodumu kwa takriban miaka minne.
“Vikundi vya shambulio vya jeshi la 2 na la 51 viliendelea kuharibu vitengo vya Vikosi vya Wanajeshi vya Ukraine vilivyozunguka katika eneo la makazi la wilaya ndogo ya Prigorodny, katika sehemu ya mashariki ya Wilaya ya Kati na katika sekta ya kibinafsi (ambapo kuna nyumba za makazi),” Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema katika taarifa.
“Mashambulio ya upande wa kaskazini yanaendelea,” iliongeza, ikisema kwamba vikosi vyake pia vilikuwa vikiwaondoa wanajeshi wa Ukraine kutoka kwa makazi kwenye ubavu wa kusini-mashariki mwa Pokrovsk na
Israel yakabidhi miili ya Wapalestina 15

Nasser Medical Complex iliyoko Khan Younis katika Ukanda wa Gaza imethibitisha kuwasili kwa miili 15 ya Wapalestina waliouawa katika Ukanda huo, ambao miili yao ilikuwa ikishikiliwa na Israel, na kukabidhiwa kupitia Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu, ikiwa ni utekelezaji wa masharti ya awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano.
Hii inafanya idadi ya miili iliyokabidhiwa jeshi la Israel kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano kufikia 285.
Makabidhiano hayo yalifanyika baada ya Hamas kukabidhi mwili wa mmoja wa wanajeshi wa Israel uliokuwa wanaushikilia usiku wa Jumanne.
Katika muktadha unaohusiana na hayo, mashahidi wa tukio hilo walithibitisha kwamba wawakilishi wa Shirika la Msalaba Mwekundu na Brigedi za Qassam, tawi la kijeshi la Hamas, walielekea eneo la Shuja’iyya mashariki mwa Mmi wa Gaza, kwa ajili ya kukamilisha operesheni ya kutafuta miili ya mateka zaidi wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
Kenya: Mvua nchini kote itaendelea kunyesha mwezi Novemba

Idara ya Hali ya Hewa ya Kenya (KMD) imetangaza kuwa mvua zitaendelea kunyesha nchini kote mwezi huu wa Novemba.
Katika mtazamo wake wa hali ya hewa, shirika hilo lilisema kuwa mvua zaidi ya wastani inatarajiwa kuendelea katika kaunti za Bonde la Ziwa Victoria, Nyanda za Juu Magharibi mwa Bonde la Ufa, na Kati na Kusini mwa Bonde la Ufa.
Vile vile, mvu ya chini ya wastani au kawaida inatarajiwa katika kaunti za Nyanda za Juu Mashariki mwa Bonde la Ufa (pamoja na Nairobi), nyanda za juu Kusini-mashariki, Pwani na sehemu kubwa ya Kaskazini-mashariki.
“Mvua itakayonyesha haitakuwa ya kiwango sawa, na vipindi vya ukame vya hapa na pale katika maeneo kadhaa ya nchi,” mtaalamu wa hali ya hewa alibainisha.
Hata hivyo, halijoto inatarajiwa kusalia joto zaidi kuliko kawaida nchini kote huku kukiwa na uwezekano mkubwa wa mafuriko katika eneo la magharibi na vipindi virefu vya kiangazi katika maeneo ya mashariki mwa nchi.
Maeneo ya Nyanda za Juu Magharibi, Mashariki mwa Bonde la Ufa na Bonde la Ziwa yamebainishwa haswa kuwa yana uwezekano wa kupata mvua za wastani, hivyo kuhitaji tahadhari kutokana na udongo ambao tayari umejaa maji.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.