Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Picha: Leon Neal/Getty/AP/picture alliance
Marekani imesema kuwa Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman atafanya ziara rasmi nchini humo tarehe 18 ya mwezi wa Novemba ambapo atafanya mazungumzo na Rais Donald Trump.
Ziara hiyo inakuja wakati ambapo Trump anaishinikiza Saudi Arabia kujiunga na orodha ya nchi ambazo zilitia saini mikataba wa Abraham, inayolenga kusawazisha mahusiano baina ya Israel na mataifa kadhaa ya Kiarabu.
Mwaka 2020 Trump alikubaliana na Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Sudan na Morocco kusawazisha mahusiano yao na Israel.
Lakini Saudi Arabia qimesita kujiunga na orodha hiyo kutokana na kukosekana kwa hatua zitakazolifanya Palestina kuwa taifa huru.
Ila katika mahojiano Jumapili iliyopita, Trump alisema ana matumaini kuwa saudi Arabia itajiunga na mikataba hiyo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.