Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Udalali ni moja ya biashara inayofanya vizuri mjini na vijini na watu ambao wenye pesa ni madalali.
Mtu yeyote mwenye bidii, uaminifu na taarifa sahihi anaweza kuanza kufanya, bila kuhitaji elimu kubwa au mtaji mkubwa wa fedha..
Kwa sasa, hata simu yako ya mkononi inaweza kukutengenezea kipato kupitia udalali. Kazi kubwa unayofanya ni kuuza taarifa ukijua kitu fulani kinapatikana wapi, basi unatafuta mteja na kufanikisha biashara.
Biashara za udalali unazoweza kufanya..
1. Spare za Magari ..Tafuta sehemu zenye bei nafuu, uunganishe na wateja.
2. Udalali wa mafundi...
Unapata kazi, unatafuta fundi, mnapatana bei, unapata kipato chako.
3. Mavazi ya designers (mfano: suti za maharusi) unganisha wabunifu na wateja.
4. Mazao ya kilimo.
Pata wakulima mikoani, tafuta wanunuzi mjini.
5. Mbao ni adimu; ukijua wapi zinapatikana, tafuta wanunuzi.
6. Udalali kariakoo au Gikomba . Bidhaa nyingi zinapatikana hapo, tumia nafasi hiyo.
7. Bidhaa za afya. Ungana na kampuni, uza bidhaa zao.
8. Sherehe na matukio. Udalali wa MC, mapambo, ukumbi n.k. Mfano kama bajeti ya MC ni Tsh 1M, mteja akipatikana kwa bei hiyo, MC anakulipa 10% ya tenda.
Mambo ya kuzingatia ili kufanikisha udalali.
1.Fanya kwa Utaalamu.. Elewa vizuri eneo unalofanya udalali.
2.Uaminifu. Kuwa mtu wa kuaminika; heshima na jina zuri ndizo mtaji wako mkubwa.
3.Jenga mitandao (Connections)..Connect na wafanyabiashara, madalali wakubwa na watu wenye mtaji.
4.Bei Sahihi…Usipandishe bei hovyo weka kiwango kinachofaa.
5.Kujitangaza.. Tangaza sana unachofanya kupitia mitandao, mabango au mdomo-kwa-mdomo..
Hatua za kuanza biashara ya udalali..
✓Chagua eneo au bidhaa unayotaka kufanyia udalali.
✓ Ijue kwa undani ili uwe mtaalamu na mtoa taarifa sahihi.
✓Tafuta wazalishaji/wenye bidhaa na ujiridhishe.
✓Jenga jina na uaminike kwa wateja na washirika.
✓Jitangaze sana ili watu wakijua wanachotaka, wakukumbuke wewe kwanza.
Udalali ni fursa halisi…
Huhitaji mtaji mkubwa, ila unahitaji uaminifu, taarifa na bidii ya kufuatilia. Kuna watu wengi waliotoka sifuri na kujijengea maisha kupitia udalali.
Usikate tamaa kwa kisingizio cha kutokuwa na mtaji anza pale ulipo, kwa kile unachoweza.
Sasa naomba uniambie unataka uanze kwa udalali gani?.
Niandikie kwenye comment ili tuweze kujadili kwa kina na nikusaidie zaidi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.