Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Saa chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu kula kiapo amezungumzia makundi ya waangalizi wa uchaguzi yalioalikwa nchini humo akisema kuwa hilo ni kutokana na mfumo wa demokrasia.
Waangalizi waliokuwepo kutoka Afrika ni pamoja na Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya nchi za Mawiza Makuu (ICGLR), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na wengineo kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Rais Samia alishukuru makundi hayo kwa maoni yao lakini akaweza wazi kuwa sio kila jambo walilotaka linaweza kutekelezwa ila Tanzania yenyewe ndio yenye uwezo wa kuamua nini cha kufanya na kunukuu maneno ya Rais wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wakati akiapishwa kuwa rais mwaka 2000.
“Nawashukuru watazamaji wetu wa kimataifa kuja kushuhudia uchaguzi wetu ulivyofanyika,walipotusifu tumepokea sifa hizo kwa nyenyekevu mkubwa. Tumesikia pia waliodhani hayakwenda saw ana mengine hata sisi wenyewe tumeyaona. Maagizo ya kutuelekeza nini cha kufanya tumeyakataa,” mwisho wa nukuu ya Rais Benjamin Mkapa iliyosomwa na Rais Samia.
Rais Samia aliongeza kuwa hakuna aliyemkamilifu duniani.
Rais Samia atoa onyo dhidi ya waliochochea vurugu

Rais Samia ametoa hotuba yake baada ya kuapishwa kama rais wa awamu ya sita nchini Tanzania.
Wakati anazungumza alikiri kuwa kipindi cha kampeni kulikuwa na migawanyiko lakini baada ya uchaguzi wote wamekuwa kitu kimoja.
“Nawasihi tuendelee kuilinda itikadi yetu ya umoja na mshikamano,” alisema Rais Samia.
Aidha, Samia amezungumzia matukio ya vurugu yaliyochangia watu kupoteza maisha, kupoteza mali ya umma na watu binafsi katika baadhi ya maeneo nchini humo.
Akikemea vikali matendo hayo alisema “kilichotokea hakiendani na taswira na sifa za Kitanzani akidai kuwa wengine waliokamatwa wakati wa vurugu hizo ni raia kutoka nje ya Tanzania.
Rais Samia ametoa onyo kwa wote waliofanya vurugu.
“Sasa tuchague lenye manufaa kwetu kwani usalama wa taifa lolote hulindwa kwa wote, kwa nguvu zote na kwa gharama zozote.”
Viongozi waliohudhuria uapisho wa Rais Samia watoa wito wa amani
Viongozi mbali mbali barani Afrika wamehudhuria hafla ya kumuapisha na kumpongeza rais wa sita wa muungano wa Tanzania Samia Suluhu eneo la Dodoma nchini humo.
Akitoa hotuba katika hafla ya uapisho wa rais Samia Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ameeleza kuwa anafurahia mshikamano wa Tanzania hasa amani na kumpongeza Rais Samia.
‘Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ametoa wito kwa wanachama wa bara la Afrika kudumisha amani ili kuimarisha uchumi.
”Viongozi wa bara Afrika tuendekeze maridhiano hasa wakati wa ghasia ili kuhakikisha uchumi hautatiziki” asema Hichilema.
Akiongezea amemtaka Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu kujumuisha wapinzani wake kwa serikali bila ubaguzi.
Samia Suluhu Hassan aapishwa kuongoza Tanzania kwa muhula wa pili

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepishwa kwa muhula wa pili chini ya ulinzi mkali, kufuatia uchaguzi uliokumbwa na ghasia na kupingwa na upinzani.
Hafla ya uapisho wake huo zinafanyika katika uwanja wa kijeshi katika mji mkuu wa Dodoma.
Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania huu ni muhula wa pili wa Rais Samia japokuwa ameongoza kwa miaka minne baada ya kumrithi mtangulizi wake Hayati John Magufuli.
Viongozi mbalimbali barani Afrika wamehudhuria ni pamoja na Naibu rais wa Kenya Kindiki Kithure, Rais wa Jamhuri ya Somalia Hassan Sheikh Mahmoud , Rais wa Zambia Hakainde Hichilema, Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, Rais wa Usumbuji Daniel Chapo na wanadiplomasia.
Samia alitangazwa mshindi Jumamosi kwa asilimia 98 ya kura.
Alikabiliwa na upinzani mdogo huku wagombea wakuu waliokuwa wakishindana nao wakifungwa au kuzuiwa kugombea.
Waangalizi wa kimataifa wameibua wasiwasi kuhusu uwazi wa uchaguzi huo, huku mamia ya watu wakiripotiwa kuuawa na kujeruhiwa.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.