Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na: Cantona Joseph|RFA

Picha: Evelyn Hockstein/REUTERS
Rais wa Marekani Donald Trump amerudia kitisho chake cha kufanya operesheni ya kijeshi nchini Nigeria kufuatia mauaji ya Wakristo nchini humo.
Hii ni baada ya afisi ya rais ya Nigeria kupendekeza mkutano ili kulitatua suala hilo.
Alipoulizwa na mwandishi wa shirika la habari la Ufaransa AFP iwapo anatafakri kupeleka majeshi Nigeria au kufanya mashambulizi ya angani, Trump alisema kuwa huenda mambo mengi yakafanyika.
Kiongozi huyo wa Marekani amedai kuwa Wakristo wanauwawa kwa wingi nchini Nigeria na kwamba marekani haitokubali hilo kuendelea kufanyika.
Trump alitoa madai hayo ya kuuwawa kwa Wakristo Nigeria katika ujumbe aliouchapisha katika mtandao wake wa kijamii wa Truth Social alipodai kuwa Ukristo unakabiliwa na kitisho katika nchi hiyo iliyo na idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika.
Nigeria ambayo ina raia wengi Waislamu katika eneo la Kaskazini na karibu idadi sawa na hiyo ya Wakristo katika eneo la kusini, inakabiliwa na mizozo kadhaa ambayo wataalam wanasema imewauwa wakristo na waislamu vilevile.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.